Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
04 Agosti 2025
04/08/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kw
-
Watoto zaidi ya 640,000 wako hatarini kufuatia mlipuko wa kipindupindu Darfur
04/08/2025 Duration: 02minZaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Selina Jerobon
-
IMF yatoa mtazamo mpya wa Uchumi wa dunia kwa mwaka 2025/ 2026
01/08/2025 Duration: 03minMnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
-
Ndoto ya Sahar ya kushamiri kimaisha yatwamishwa na mashambulizi ya Israeli Gaza
01/08/2025 Duration: 02minHarakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula. Ripoti ya Selina Jerobon inayotokana na video iliyochapishwa mtandao wa X na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipaletina, UNRWA, inafafanua zaidi.
-
01 AGOSTI 2025
01/08/2025 Duration: 10minHii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushi
-
Maspika wa Mabunge wapitisha azimio la kihistoria Geneva, Uswisi
01/08/2025 Duration: 02minMkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo.
-
Fursa zipo, vijana wajitokeze kusongesha malengo ya maendeleo endelevu - Kapwani
31/07/2025 Duration: 05minJukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025. Jukwaa hili lilifanyika kwa siku 4 likileta pamoja vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani na wadau wa maendeleo na uchumi ili kujadili changamoto zinazowakabili vijana na kutoa mapendekezo ya kuboresha dunia kuelekea usawa na maendeleo endelevu chini ya Ajenda ya 2030 au Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Miongoni mwa vijana walioshirikki ni Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania. Akizungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa hii, Bi. Kapwani alianza kwa kuelezea alichokuwa anasongesha mbele baada ya kushiriki mkutano wa Zama Zijazo au Summit of The Future uliopitisha Mkataba wa Zama Zijazo au PACT OF THE FUTURE mwezi SEptemba mwaka jana 2024.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno MTAGARUKI
31/07/2025 Duration: 55sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.
-
31 JULAI 2025
31/07/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mik
-
Siku ya kimataifa ya urafiki, je wewe wapenda kuwa na rafiki wa aina gani?
30/07/2025 Duration: 03minUmoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi ya urafiki katika kujenga amani, utulivu na kusongesha maendeleo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya mataifa, mwaka 2011 kupitia Baraza lake Kuu, ulitenga Julai 30 kuwa siku ya urafiki duniani. Umoja wa Mataifa unasema katika wakati ambapo kelele za mgawanyiko zinazidi kuwa kubwa — zikiendeshwa na vita, migogoro, ukosefu wa usawa, na hofu — urafiki unaonekana kuwa wa kishujaa kutokana na unyenyekevu wake. Urafiki huanza na kitu cha utulivu zaidi: mazungumzo, wakati wa pamoja, utayari wa kuonana si kama wageni bali kama wasafiri wenza katika safari ya utu. Je huko Kenya, mkazi mmoja wa Kaunti ya Kajiado, urafiki kwake ni nini? Kelvin Keitany wa Redio washirika Radio Domus amefunga safari na kutuandalia makala hii.
-
IFAD: Kilimo chazaa matunda Rwanda: wakulima wadogo wajikwamua
30/07/2025 Duration: 02minKatika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Sharon Jebichii na taarifa zaidi.
-
30 JULAI 2025
30/07/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiy
-
Tanzania kuanza kutekeleza mpango wa WHO wa Beat the Heat
30/07/2025 Duration: 01minTanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.
-
29 JULAI 2025
29/07/2025 Duration: 11minHii leo jaridani utasikia muhtasari wa habari utakaoangazia hali ya uhaba wa chakula Gaza, mkutano wa maspika wa bunge duniani na mkutano wa tabianchi na afya. Katika jarida pia utasikia mada kwa kina inayoangazia siku ya kimataifa ya marafiki duniani ambayo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2011 ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Julai. Vijana kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino nchini Tanzania - SAUT wanajadili umuhimu wa siku hii.
-
Türk ataka Israeli ishinikizwe iondoke maeneo inayokalia ya wapalestina
28/07/2025 Duration: 01minKamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKamishna Turk ameyasema hayo katika tarifa yake aliyoitoa kwa njia ya video kabla ya kuanza kwa mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani unaolenga kujadili Suluhu ya kudumu kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina ambao umedumu kwa miongo kadhaa sasa.Turk amesema: “Ninahimiza hatua za haraka za Israel kukomesha uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kwa pande zote kufanyia kazi maendeleo yanayoonekana kuelekea suluhu ya Serikali mbili.”Akatoa angalizo kwa zile nchi zitakazo shindwa kuweka shinikizo kwa Israel kukomesha mauaji huko katika Ukanda wa Gaza.“Nchi ambazo zinashindwa kutumia n
-
Mauaji ya raia Komanda, Ituri, MONUSCO yalaani waasi wa ADF
28/07/2025 Duration: 01minMONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Taarifa iliyotolewa na MONUSCO jijini katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa imeeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa za uhakika, shambulio hilo lililofanywa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) limesababisha vifo vya raia wasiopungua 43 (wanawake 19, wanaume 15 na watoto 9).Inaripotiwa kuwa waathirika wengi waliuawa kwa kutumia silaha za jadi wakiwa ndani ya nyumba ya ibada. Watu kadhaa walitekwa nyara. Nyumba na maduka pia yalichomwa moto, jambo ambalo limezidisha zaidi hali mbaya ya mazingira ya kibinadamu ambayo tayari ni ya kutisha katika jimbo hilo.Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mata
-
28 JULAI 2025
28/07/2025 Duration: 09minHii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mauaji Ituri, DRC; Haki za binadamu hususan suala la Israeli kukalia Palestina kimabavu; Mifumo ya kuzalisha chakula; Mradi wa umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola huko Bidibidi, Uganda. MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKatika makala Sabrina Said anakupeleka Addis Ababa nchini Ethiopia, kumul
-
Ubia wa Serikali, UNICEF na Wakfu wa Gates Pemba, nchini Tanzania warejesha afya ya wajawazito na watoto
25/07/2025 Duration: 03minHuko Pemba, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, Mpango mpya wa afya ya mama unawasaidia wanawake wajawazito kukabiliana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya. Kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na kwa msaada wa kifedha kutoka Wakfu wa Gates, zaidi ya wanawake 16,000 sasa wanapata huduma bora kupitia Virutubisho vya Madini Mbalimbali (MMS) na huduma zilizoboreshwa za kliniki za wajawazito. Assumpta Massoi amefuatilia mradi huo kupitia video ya UNICEF TAnzania.
-
Hali ya Gaza ni janga la maadili linalotikisa dhamira ya ulimwengu - Guterres
25/07/2025 Duration: 01minKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kuwa mateso yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni zaidi ya janga la kibinadamu – ni janga la maadili linalopasua dhamira ya jumuiya ya kimataifa. Leah Mushi na maelezo zaidi.
-
25 JULAI 2025
25/07/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza, na Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda nchini Uganda, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kuwa mateso yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni zaidi ya janga la kibinadamu – ni janga la maadili linalopasua dhamira ya jumuiya ya kimataifa.Leo, tarehe 25 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika, ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu: “Kuinuka Pamoja: Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika Wakiongoza kwa Nguvu.” Idhaa ya Umoja wa Mataifa imefanya mahojiano na Patricia Da Silva, Mratibu wa Kimataifa wa Timu ya Hakuna Kumwacha Yeyote Nyuma katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA na akafafanua kidogo siku hii inabeba nini hasa. Makala inatupeleka Pemba, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, ambapo mpango mpya wa afya ya mama u