Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
13 AGOSTI 2025
13/08/2025 Duration: 09minJaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nch
-
Tunatiwa hofu kubwa na kitendo cha Besigye kuendelea kunyimwa dhamana Uganda
13/08/2025 Duration: 02minOfisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
12 AGOSTI 2025
12/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain, wadau kwa kushirikiaa na ofisi ya Uwekezaji na Uendelezaji Teknolojia, ITPO ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO wanachukua hatua kuondolea wanawake umaskini kwa kuimarisha talanta walizonazo. Mengine ni kama yafuatayo..Leo ni siku ya Kimataifa ya vijana duniani maadhinisho yanafanyika jijini Nairobi nchini Kenya chini ya ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia vijana ujumbe maalum akisema “Kwa kijana: Sauti yako, mawazo yako na uongozi ni muhimu.”Je, vijana wanasemaje kuhusu siku hii? Kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania, Sabrina Saidi wa Idhaa hii amezungumza na baadhi yao.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP limepokea zaidi ya dola milioni 2 kutoka Japan kwa ajili ya msaada wa chakula nchini Malawi. Kwa msaada huu WFP inatarajia kusambazana tani 1970 za mahindi katika msimu wa mwambo kwa mwaka 202
-
Jukwaa Biashara lafungua masoko kwa bidhaa za wakimbizi Kakuma, Kenya
11/08/2025 Duration: 03minMakala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.
-
Kuuawa kwa waandishi wa habari 6 katika ukanda wa Gaza, viongozi wa mashirika ya UN walaani
11/08/2025 Duration: 02minKufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo. Sabrina Said na taarifa zaidi.
-
11 AGOSTI 2025
11/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughu
-
UNHCR Tanzania inaendesha zoezi la tathmini ya wakimbizi kutoka Burundi
11/08/2025 Duration: 01minMoja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii.
-
Ajira ngumu usichague kazi, chupa ni mali - Hauwa
08/08/2025 Duration: 03minHuko mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.
-
08 AGOSTI 2025
08/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza, na mradi wa mlo shuleni unaowezesha watoto kuendelea na masomo nchini Uganda. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu.Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Makala inakupeleka Mtwara, kusini mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na
-
OHCHR: Israel isitishe mara moja mpango wa kulitwaa kijeshi eneo lote la Gaza
08/08/2025 Duration: 01minKamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
Mgao wa mlo wavutia wanafunzi nchini Uganda kujifunza zaidi
08/08/2025 Duration: 01minMradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Sabrina Moshi na maelezo zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."
07/08/2025 Duration: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."
-
07 AGOSTI 2025
07/08/2025 Duration: 10minJaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpang
-
Ukame unavyobadili ratiba ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama
06/08/2025 Duration: 02minBado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado. Kelvin Keitany na maelezo zaidi.
-
06 AGOSTI 2025
06/08/2025 Duration: 09minJaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, K
-
Umoja wa Falme za Kiarabu wafanikisha vifaa vya matibabu ikiwemo damu kuwasili Gaza
06/08/2025 Duration: 02minLeo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Leah Mushi na taarifa zaidi.
-
UN yarejelea wito wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza
06/08/2025 Duration: 01minIkiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban. Anold Kayanda na tarifa zaidi.
-
05 AGOSTI 2025
05/08/2025 Duration: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva
-
Kituo kipya cha kikanda cha SDGs Asia chazinduliwa Kazakhstan
04/08/2025 Duration: 03minUmoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan. Anold Kayanda anafafanua zaidi.
-
Raia wanaendelea kuuawa katika ukanda wa Gaza wakihaha kusaka chakula
04/08/2025 Duration: 02minSimulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula. Simulizi zaidi anayo Assumpta Massoi.