Habari Za Un
Türk ataka uwajibikaji wa vikosi vya usalama Nepal na waandamanaji wazingatie kanuni
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:49
- More information
Informações:
Synopsis
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, akizungumza mjini Geneva amesema“nimeshtushwa na ongezeko la ghasia nchini Nepal ambalo limesababisha vifo kadhaa na kujeruhi mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali.”Katika siku za karibuni, maandamano yaliyoanzia katika mji mkuu Kathmandu sasa yamesambaa katika miji na vijiji vya Nepal, yakiacha barabara zikifunikwa na mabaki ya vitu vilivyoteketezwa kwa moto na kulazimisha maduka kufungwa pia kuhofia usalama.Kwa mujibu wa duru za habari maandamano hayo yanayoo nngozwa na vijana wa kati ya umri wa miaka 13 hadi 28 au Gen Z yameshakatili Maisha ya takribani watu