Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:01:58
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episodes

  • Mazishi ya papa Francis huko vatican, DRC na Rwanda zakubaliana kuelekea amani

    26/04/2025 Duration: 20min

    Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia mazishi ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, DRC na Rwanda zatia saini makubaliano kuhusu njia ya kupatikana amani ya mashariki mwa Congo, siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa oktoba, ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko China, hali ya vita ya Sudan, vita ya Ukraine na huko Gaza Israeli, ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.

  • Vita ya Sudan kuingia mwaka wa tatu, Joseph Kabila arejea nchini DRC

    19/04/2025 Duration: 20min

    Vita ya sudan Kuingia katika mwaka wa tatu wiki hii, Kenya yatangaza marufuku ya biashara ya figo baada ya ufichuzi, rais wa zamani wa DRC arejea nchini aliwasili mjini Goma huku Marekani ikiitaka nchi ya Rwanda kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo, tumeangazia siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa Oktoba, kule Sahel na wito wa rais wa Ghana wiki hii akiwataka viongozi wa nchi hizo kuungana pamoja na pia mkutano wa Paris kuhusu hatima ya vita ya Ukraine

  • Kiongozi wa Chama cha upinzani Tanzania Chadema ashikiliwa kwa uhaini, hali ya DRC

    12/04/2025 Duration: 20min

    Matukio ya wiki: kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania, Tundu Lisu, maadhimisho ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda mwaka 1994, mafuriko jijini Kinshasa huko DRC, hali ya sudan Kusini kutokana na kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, uchaguzi wa Gabon, na pia mzozo wa kibiashara kati ya Marekani na mataifa mengine ulimwenguni ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.

  • Ziara ya rais wa Uganda nchini Sudan kusini, waasi wa M23 wajiondoa Walikale

    05/04/2025 Duration: 20min

    Miongoni mwa matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, iliyotangulizwa na ziara ya wajumbe wa Umoja wa Afrika, nchini Sudan Kusini baada ya makamu wa rais wa nchini hiyo kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwake, kule DRC waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waripotiwa kujiondoa katika mji wa Walikale mokowani Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, tunaangazia Kenya, Uganda, nchi za Afrika mashariki na magharibi pia kwengineko duniani 

page 2 from 2