Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Sanaa ya uchoraji katika Visiwa vya Zanzibar
08/03/2025 Duration: 20minWachoraji visiwani Zanzibar walia na gharama za kupata maeneo ya kunadi kazi zao za Sanaa hiyo, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mchoraji maarufu visiwani humo Jamal.
-
Muziki wa Taarab na Zanzibar Hertage Ensemble
01/03/2025 Duration: 20minTaarab Asilia ni Miongoni mwa Miziki ya kale zaidi katika Mwambao mwa Bahari ya Hindi, Zanzibar Taarab Hertage Ensemble ni miongoni mwa Makundi ya Muziki huo kutoka Visiwani Zanzibar, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Tamasha la Sauti za Busara linalofanyika kila mwezi Februari Zanzibar
01/02/2025 Duration: 20minWasanii wa Muziki Afrika na Duniani kote wanakutana visiwani Zanzibar kufurahia uzuri na Upekee wa Muziki, wageni mbalimbali hukusanyika kushuhudia Tamasha la Sauti za Busara kila ifikao mwezi Februari.
-
Mfahamu Leo Mkanyia Mwanamuziki wa Muziki wa Asili kutoka Tanzania
25/01/2025 Duration: 20minWanamuziki wa Muziki wa asili wamebadili vionjo vya asili wakijumuisha na vionjo vya Kisasa ili kuupaisha Muziki Kimataifa, Steven Mumbi amezungumza na Leo Mkanyia Mwanamuziki wa Muziki wa Asili kutoka Tanzania